AFCON 2017 FAINALI: HIVI NDIVYO CAMEROON WALIVYOSHEREHEKEA USHINDI DHIDI YA MISRI..
Ilikuwa ni siku ya furaha nderemo na shamrashamra katika usiku wa February 5, siku ambayo mchezo wa fainali ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2017 ulichezwa, mchezo wa fainali ya AFCON 2017 ulikuwa unazikutanisha timu za Misri dhidi ya Cameroon, lakini Cameroon wamefanikiwa kufuta uteja kwa kufungwa fainali mbili na Misri.
Cameroon wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1, Nicolas N’koulou alifunga goli la kusawazishia Cameroon dakika ya 58 baada ya Mohamed Elneny kuifungia Misri goli la uongozi dakika ya 22, Vincent Aboubakar ndio alizima ndoto za Misri baada ya dakika ya 88 kufunga goli la ushindi.
Ushindi huo unakuja baada ya Cameroon kufumgwa fainali mbili za AFCON na Misri, alifungwa fainali ya AFCON 2008 goli 1-0 Mohamed Aboutrika akifunga goli hilo, lakini walipoteza fainali ya AFCON 1986, Cameroon wanakuwa wamechukua taji lao la tano la AFCON wakati Misri wanabakia na rekodi yao ya kuchukua mataji nane ya AFCON.
Rekodi nyingine zilizowekwa katika AFCON na Cameroon ni kuwa inakuwa timu ya kwanza kuwahi kuifunga Misri goli katika fainali za AFCON baada ya Ethiopia, huku kocha wa Misri Hector Raul Cuper akiendeleza rekodi yake mbovu kwa kupoteza fainali yake ya sita katika soka akiwa kama kocha wa timu tofauti.credit:
millardayo.com
No comments
+255716829257