Habari mpya

Rais Magufuli atengua uteuzi wa January Makamba, Simbachawene na Bashe wateuliwa

Rais John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa January Makamba ambae alikua Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira na sasa Waziri mpya kwenye kitengo hicho atakua George Simbachawene, Rais JPM pia amemteua Mbunge Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo kuchukua nafasi ya Innocent Bashungwa ambae aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. 
Kwenye hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi Dr. Martin Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ambapo ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.
Uteuzi wa Viongozi hawa unaanza leo July 21 2019.

No comments

+255716829257