JE TOFAUTI ZA KIFIKRA NDIZO ZINAZOTOFAUTISHA AINA YA WAPENZI TUNAOWAPENDA??
BINADAMU wote ni sawa lakini
tunatofautiana kimawazo, fikra, kiutendaji, kipawa nk. Haya yanathibitika sana
unapozingatia mitazamo mbali mbali mfano katika kufuatilia fikra za Mwanafalsafa
aliyekuwa maarufu sana kwa uchambuzi wa fikra na mawazo ambaye alikuwa anaitwa
Plato.
Katika kazi yake ya "Republic"
Plato alisema kuwa kila binadamu ameubwa tofauti kutokana na wengine kuwa na
akili nyingi ambaye yeye aliwaita "golden boy" ambao
yeye hawa aliwaelezea kuwa ni wale wanaweza kuwa viongozi wa nchi yaani
(Philosphers, Gvern Planners and Rulers)
Wengine wanaakili ya kawaida "Silver
boy" kwa mujibu wa Plato hawa ni wale wanaotakiwa kuwa walinzi wa
nchi yaani askari jeshi na polisi pia alisema kundi la mwisho wa wale ambao
wanaakili finyu "Iron Boy "hawa Plato alisema kwa
kuwa wanauwezo mdogo wa kupambanua mambo kazi yao ni kulima na kuwa wazalishaji
wa bidhaa za nchi na kufanya kazi zingine ndogondogo.
Hii inadhihirika pale ninapojaribu
kufanya uchunguzi wangu na kugundua kuwa kumbe hata katika suala la mapenzi na mahusiano, binadamu tuko tofauti wengine wanapenda wapenzi wao wawe wanene na wengine wembamba, vile vile wengine hupendelea weupe na wengine weusi.
Katika msingi wa makabila, wapo wanapenda
kabila fulani, kama wachaga, wapare, wasukuma na mengineyo mengi. Hali kadhalika wapo wanapendelea wenza wao wawe wasomi na kinyume chake. Hapa falsafa ya Plato inaonekana kudhihirika wazi wazi kuwa binadamu wanatofautiana kimawazo na jinsi ya kufikiri na kuchanganua mambo.
Je, katika kwa mtazamo wako ndugu msomaji wa makala hii unaona
je??..
No comments
+255716829257