Makamu wa rais Afrika Kusini akosoa kufutwa kazi waziri wa fedha
Makamu wa rais nchini Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameitaja hatua ya kufutwa kazi waziri wa fedha Pravin Gordhan kuwa isiyokubalika.
Kufutwa kazi kwa Gordhana kumesababisha masoko ya hisa kushuka kwa asilimia 5.
Bwana Gordhan alionekana kama mpinzani mkubwa wa ufisadi kwenye uongozi ambao umekosolewa vikali.
Aikuwa mmoja wa mawaziri waliofutwa kazi wakati Rais Jacob Zuma, alilifanyia mabadiliko baraza la mawaziri.
- Zuma amfukuza kazi waziri wa fedha Pravin Gordhan
- Donald Trump na Uhuru Kenyatta wazungumza kwa Simu
Bwana Ramaphosa alikiambia kituoa cha habari cha SABC kuwa hatajiuzulu kufuatia kufutwa kwa mawaziri hao bali ataendelea kuwatumikia watu.
Pravin Gordhan alitajwa na wengi kama mtu mwenye tajriba ya kusimamia uchumi.
Alikuwa akizuia matumizi makubwa ya serikali na kukataa wito wa rais wa kutaka matumizi ya serikali kuongezwa.
Huu ndiyo duru ya pili bwana Gordhan anahudumu kama waziri wa fedha baada ya kuhudumu kwanza kati ya mwaka 2009 na 2014.
Aliteuliwa mwaka 2015 kuchukua mahala pa David van Rooyen. Uteuzi wa bwana Van Rooyen ulikumbwa na utata na alihudumu kama waziri wa fedha kwa muda wa wiki moja.
No comments
+255716829257