SHERIA INASEMAJE KUHUSU FAO LA WATEGEMEZI WA MFANYAKAZI ALIYEFARIKI??..
Sheria ya
Hifadhi ya Taifa ya Jamii, 1997 inatoa fao la wategemezi wa mfanyakazi
aliyefariki wategemezi hawa ni pamoja na mjane/kizuka na watoto chini ya umri
wa miaka 18 (umri wa miaka 21, ikiwa ni mwanafunzi, hakuna kikomo cha mlemavu).
Ikiwa mfanyakazi anafariki na ametimiza matakwa ya haki kwa umri wa uzee au
pensheni batili au alikuwa anaipata tayari, wategemezi wake wanahaki ya ruzuku
ya wasaliaji.
Kama
hakuna watoto tegemezi, 100% ya pensheni ya marehemu itaenda kwa mjane/mgane wa
marehemu.
Pensheni
hii italipwa kwa miaka 2 kama mjane/mgane ana umri chini ya miaka 45 au hana
mtoto chini ya miaka 15 wakati wa kifo cha mfanyakazi aliye na bima. Endapo
kuna watoto tegemezi, mjane/mgane atapewa 40% ya pensheni na 60% itagawanywa
kati ya watoto. Pensheni ingawanywa sawia ikiwa kuna zaidi ya mjane/mgani
mmoja.
Kama
hakuna mjane/mgane, 100% ya pensheni itagawanywa kwa watoto tegemezi (Chini ya
miaka 18 au 21 kama bado anahudhuria masomo).Pensheni ya wasaliaji inapatikana
milele ay hadi ndoa ya mjane/mgane wa zaidi ya miaka 45.
Pesa zenye thamani ya mara 24 ya pensheni kwa mwezi zitalipwa kwa mara ya kwanza na baada ya hapo itafuatiwa na pensheni ya mwezi. Kiwango cha chini cha pensheni ni 80% ya Viwango vya chini cha mshahara vya kisheria. Ridhia ya msaliaji na ridhia ya mazishi pia inalipwa kwa wategemezi.
Na endapo hakuna mgane/mjane, wala watoto tegemezi basi 100% itagawanywa kwa wazazi wa marehemu.

Chanzo: §
33-36 ya Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii 1997
No comments
+255716829257