Habari mpya

TP Mazembe na Mamelodi Sundowns wameshindwa kutamba dhidi ya timu za Kaskazini

Baada ya kuchezwa kwa michezo ya kwanza ya nusu fainali ya CAF Champions League na kuona timu za Wydad Casablanca ya Morocco ikiifunga Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini 2-1 na Esperance ya Tunisia kuifunga TP Mazembe 1-0, wengi waliamini Mamelod na TP Mazembe wakirudi kucheza kwao watapindua matokeo.
Mambo yamekuwa tofauti licha ya kuwepo kwa tofauti ndogo ya magoli lakini game hizo zote mbili zimemalizika kwa matokeo ya sare 0-0 na kujikuta TP Mazembe na Mamelodi wakiaga mashindano yao hayo kutokana na kushindwa kupindua matokeo, huku Bingwa mtetezi Esperance akiingia fainali dhidi ya Wydad Casablanca.
Hivyo mchezo wa kwanza wa fainali ya CAF Champions League kati ya Eperance ya Tunisia dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco utachezwa May 24 2019 na marudiano May 31 2019, michezo hiyo inachezwa mapema ili kutoa nafasi kwa wachezaji wa timu ya taifa kuungana na timu zao katika maandalizi ya fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2019 zinazochezwa June 21 hadi July 19 2019 nchini Misri.

No comments

+255716829257