Habari mpya

IJUE HATI YA MAANDISHI YA AJIRA..

Image result for HATI YA MAANDISHI YA AJIRA
Sheria ya kazi ya Tanzania inahitaji kwamba wafanyakazi wapewe mkataba ulioandikwa wa ajira wanapoanza ajira isipokuwa kwa wale ambao wanafanya kazi chini ya siku 6 kwa mwezi kwa mwajiri fulani. Huenda mkataba wa ajira ukuwa wa kipindi chenye kikomo au kisichokuwa na kikomo au kazi maalum. Lazima mkataba wa ajira uwe umeandikwa ukiwa unampa mfanyakazi huyo kufanya kazi nje ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania.
Mkataba wa ajira lazima ueleze maelezo yafuatayo. Jina, umri, anwani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi; mahali pa kuajiriwa; ufafanuzi wa kazi; tarehe ya kuanza; aina na muda wa mkataba; mahali pa kazi; saa za kufanya kazi; ujira, mbinu ya hesabu yake, na maelezo ya faida aiu malipo ya aina yoyote, na suala lingine lililofafanuliwa. Hata hivyo, ikiwa vipengele hivi vimetolewa tayari katika mkataba wa ajira, huenda mwajiri asijaze hali iliyoandikwa ya vipengele vya ajira.
Lazima mwajiri ahakikishe kwamba vipengele vyote vilivyoandikwa vimefafanuliwa wazi kwa mfanyakazi kwa njia inayoeleweka na mfanyakazi. Ikiwa kuna mabadiliko yoyote katika kipengele chochote kilichoandikwa, mwajiri anahitajika kupitia upya vipengele vilivyoandikwa kwa kushauriana na mfanyakazi ili kuangazia mabadiliko hayo. Lazima mwajiri amfahamishe mfanyakazi kuhusu mabadiliko hayo kwa kuandika.
Mwajiri anawajibika kuweka vipengele vilivyoandikwa kwa kipindi cha miaka mitano baada ya ajira kuisha. Ikiwa mwajiri atashindwa kutoa mkataba ulioandikwa katika kesi zozote za kisheria, mzigo wa kuthibitisha au kukataa masharti fulani ya ajira uko kwa mwajiri. Kila mwajiri lazima aonyeshe taarifa ya haki ya wafanyakazi katika mahali panapoonekana.
Chanzo: Sehemu ya 14-16 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004.


No comments

+255716829257