ZIJUE SABABU ZA MWANAUME KUSHINDWA KUMPA MIMBA MWANAMKE
mwanamke pekee ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha anapata mimba na ikitokea akakaa muda mrefu kwenye ndoa bila hilo kutokea, basi jamii inamtupia lawama wakiamini tatizo ni lake na siyo mumewe.
Ukweli kitaalamu ni kwamba tatizo linaweza kuwa kwa mwanaume au mwanamke au wote wawili wana matatizo, tena makubwa.
MWANAUME KUSHINDWA KUMPA MIMBA MWANAMKE
Mara nyingi mwanaume kushindwa kumpa mimba mwanamke kunatokana na matatizo ya kuzaliwa nayo kama vile korodani kushindwa kushikana vizuri Undrescended test, hii hutokea baada ya vichocheo (Hormone) kupata hitilafu na kuweza kuleta matatizo ya uzalishaji wa mbegu za kiume ambazo kitaalamu huitwa Spermatogensis ingawa vitu kama mrija wa kutolea mbegu unakuwepo lakini huwa hakuna mbegu zinazozalishwa.
Tatizo lingine ni la kimaumbile ambapo kwenye mrija wa kutolea mbegu, pamoja na mkojo, yaani Urethra huota sehemu ya chini ya uume, hivyo kusababisha mbegu kutoweza kufika sehemu ya ndani ya uke, tatizo hili kitaalamu huitwa Hypospadias.
Tatizo lingine linalofanya mwanaume kushindwa kumpa mimba mwanamke ni korodani kupata joto sana, kitaalamu huitwa Termal Factor.
Hali hiyo huleta hitilafu kwenye korodani na kusababisha mbegu zisitoke zikiwa na afya nzuri. Tatizo hili huwakumba zaidi madereva wanaosafiri safari ndefu kwa zaidi ya siku mbili.
Sababu nyingine ni magonjwa ya zinaa kama yale yanayosababishwa na bakteria aina ya Chlamydia na kusababisha tatizo la uzazi kwa mwanaume au tatizo la tezi za shingoni Mumps ambazo huathiri korodani na kusababisha mbegu kutozalishwa, hivyo kusababisha tatizo la uzazi kwa mwanaume.
Matatizo mengine, wanaume huyapata kutokana na kuvuta sigara kwa wingi, kunywa pombe kupita kiasi kwani vitu hivyo husababisha hitilafu ya kuzalisha mbegu.
Lakini pia matatizo yanayodhoofisha mwili kama utapiamlo, pia husababisha hitilafu ya uzalishwaji wa mbegu mwilini. Vilevile matatizo ya kurithi ambayo kitaalamu huitwa Chromosomal huweza kusababisha mwanaume asiweze kumpa mimba mwanamke kwani mbegu za kiume huwa chache na hazitoshelezi kusababisha mimba.
Wanaume ambao wamepigwa miale kama ya Ex ray, CT Scan, matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, dawa za presha, dawa za kuzuia degedege pia huathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume.
Tatizo lingine ni ukosefu wa nguvu za kiume ambao kitaalamu huitwa Erectle Dysfunction au mwanaume kuwa hanithi Impotence kunaweza kusababisha ashindwe kumpa mimba mwanamke
No comments
+255716829257