Habari mpya

IFAHAMU ASILI YA WAPARE..

WAPARE NA UPARE.
Tanzania ni nchi yenye makabila zaidi ya 120 lakini katika makala hii endelevu nitaanza kwa kuchambua kabila la wapare, je wapare ni kina nani?  Asili yao ni nini? Wanaishi wapi? Wanajishughulisha na nini? Lakini pia ni zipi mila na desturi zao?
Ndugu msomaji ungana na mwandishi wako Ramadhani Gidion katika  kuifwatilia makala hii endelevu itakayokuchambulia mila na desturi za makabila mbalimbali ndani ya Tanzania pamoja na kutambua vivutio vya asili vinavyopatikana katika mazingira yao.
Kabila la wapare linapatikana mkoani Kilimanjaro kaskazini mwa Tanzania katika wilaya ya Same na Mwanga japo wapo wapare waishio maeneo ya Moshi kama vile chekereni,himo,uchira, mabungo na moshi mjini, vilevile wanaishi wilayani Hai kwenye maeneo kama Rundugai na mto weruweru.Mkoani Tanga wapare wanaishi zaidi lushoto katika maeneo ya Bumbuli na Mavumo.
Asili ya wapare inasemekana ni Taveta nchini Kenya ambako waliishi huko zaidi ya karne moja na nusu iliyopita wakijulikana kwa jina la “waasu” kabla ya kuingia Tanganyika kupitia mpaka wa Taveta.Historia inaeleza kuwa wapare wa mwanzo walifikia katika miteremko ya mlima kilmanjaro wakiongozwa na machifu wao mashuhuri kama vile mfumwa (chief)  Boazi Mashambo ambako waligombana na wenyeji ambao ni wachaga na kuhamia milima ya Same na Mwanga ambayo saivi inafahamika kama milima ya upare.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7qqSKP27PrK5xbldyLbiPvDT5jYsfKsvQ9R3IMT1j2JMJkySQjvU5R9J6TR5atrM-dmV5K8Su3VQbrfwlXZpf31otDc_7CZLU4mN-bObDFFmEtKz-_NZ_J9K8mroGktHe6MWhUEBS_Y3o/s400/MADEVENI+TRIP+024.jpg

Wapare wamegawanyika katika makundi mawili wapo wapare wa kaskazini (vampare va mpare ya ughu) hawa huishi wilayani Mwanga kwenye meneo ya ugweno ambao huongea lugha ijulikanayo kama “kigweno” na wapo wanaishi maeneo ya Usangi hawa hutumia lugha ya kipare. Kundi la pili ni wapare wa kusini (vampare va mpare ya kusea) hawa huishi wilayani Same huzungumza kipare jopo kinatofutiana matamshi (lafudhi) na wapare wa usangi.
Kabila hili hujihusisha zaidi na kilimo cha mahindi,maharagwe, mpunga, na vitunguu hasa kwenye mabonde maarufu yaliyojaliwa maji na rutuba kama vile bonde la Ruvu,kisiwani, maore na Ndungu wilayani Same vilevile maeneo ya Ugweno na Usangi wilayani Mwanga ambapo kilimo cha migomba kimeshamiri zaidi.Same milimani pia kwenye maeneo ya Mbaga na Gonja kilimo cha migomba na nafaka kama maharagwe na mahindi hutegemewa zaidi kama zao la chakula katika maisha ya kila siku.Katika eneo la mamba miamba na Kanza husifika zaidi kwa kilimo cha tangawizi pia yapo mabwawa na madimbwi mbalimbli yatumikayo katika shughuli za uvuvi kama vile bwawa la nyumba ya mungu, bwawa la ndungu na dimbwi la msangeni.


Mbali na uwepo wa aridhi nzuri yenye  rutuba kwa kilimo katika milima na mabonde ya upare pia vipo vivutio vya utalii wa asili katika maeneo hayo ikiwemo mito maarufu kama vile Hingilili,Rika,Nakombo, Mhoke vuta, Yongoma, Mwetanano pamoja na maporomoko yanayosemekana kuwa marefu kuliko ya ziwa Victoria (Victoria falls) maarufu kama “Ndurumo” yapatikanayo eneo la Gonja Bombo.

                                                             
Hali kadhalika upareni kuna hifadhi kubwa ya Taifa ya Mkomazi,Bwawa la Kalimawe na Nyumba ya mungu,milima ya Kindoroko,mokanda  na Masheko vudee ndolwa.Pia kuna majabali makubwa yavutiayo wataalii kuja kutizama kama lile la Malameni linalopatikana Mbaga Manka ambalo zamani inasemekana zilikua zikisikika sauti za wasichana watatu ndani ya jiwe hilo vilevile kuna jabali la Mhewe linalopatikana vudee ndolwa.

Usikose mwendelezo wa makala hii……

No comments

+255716829257