Slovakia yaichapa Urusi 2-1 michuano ya Euro..
Wakicheza ndani ya Stade Pierre Mauroy Mjini Lille huko France, Slovakia wameitandika Urusi 2-1 katika Mechi ya Kundi B la EURO 2016 na hizi ni Mechi za Pili kwa kila Timu.
Slovakia waliongoza 2-0 hadi Mapumziko kwa mabao ya Vladimir Weiss katika Dakika ya 32 alipotengenezewa na Kiungo wa Napolo Marek Hamsik na goli la Pili dakika ya 45. Russia, ambao wana kitanzi shingoni baada ya kuhukumiwa na UEFA adhabu iliyositishwa ya kutupwa nje ya EURO 2016, kutokana na fujo za mashabiki wao kwenye mechi yao ya kwanza na Uingereza, walipata bao lao moja dakika ya 80 mfungaji akiwa Denis Glushakov.
Lakini goli hilo lilileta tukio la mashabiki wao kufyatua fataki uwanjani na sasa inabaki juu ya UEFA kuamua Russia wabaki France au la. Ikiwa UEFA itawabakisha, basi Urusi wanapaswa kuifunga Wales katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi B ili kusonga mbele.
Nao Slovakia, ambao walifungwa na Wales katika mechi yao ya kwanza, wanapaswa kuifunga Uingereza katika Mechi yao ya mwisho ili wafuzu. Na Wenyeji Ufaransa wamepata ushindi wa 2-0 na kutinga Raundi ya ttoano ya timu 16 wakiwa na mechi moja mkononi walipoifunga Albania katika Mechi ya Kundi A la EURO 2016, iliyochezwa huko Stade Velodrome, Marseille. Albania waliwamudu vyema France kwa Dakika 89 na ndipo Antoine Griezmann, alietokea Benchi, kuwatoboa kwa Bao la Kichwa na kwenye Dakika za Majeruhi, Dakika ya 95, Dimitri Payet kufunga Bao la Pili. Baada ya Mechi 2 France wapo juu Kundi A wakiwa na Pointi 6 wakifuata Uswisi wenye Pointi 4, Romania 1 na Albania 0.
chanzo: BBC
No comments
+255716829257