SALIM BIMANI: MAALIM SEIF HAKUTOA KAULI MBAYA KWA LIPUMBA..
Baadhi ya
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii June 15 2016 vimeamka na
habari yenye kichwa cha habari ambacho kimenukuu Katibu Mkuu wa chama
cha CUF, Maalim Seif akisema ‘Prof. Lipumba asahau uenyekiti CUF’.
June 15 2016 chama cha wananchi CUF kupitia kwa kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi, Salim Bimani amekanusha taarifa
zilizoripotiwa na vyombo vya habari ambapo taarifa hiyo imesema
kwamba Taarifa hii ni uongo na katibu hajaitoaa. Hii ni miongoni mwa
propaganda zinazotengenezwa na watu wasio na malengo mema na chama,
wakijua fika kwamba maamuzi ya chama hayafanywi na mtu bali vikao vya
chama.
Taarifa
imeongeza kuwa maoni na msimamo wa Katibu mkuu Maalim Seif ambaye yuko
Marekani ni kwamba wanachama wanasubiri maamuzi ya vikao vya chama
vitaamua mambo mbalimbali yanayoendelea na yanayotokea na vitatangaza
maamuzi yake kwa wote.
Chama
hicho kimetoa Rai kwa wanahabari kuwa makini sana na vyanzo vya taarifa
mbalimbali wanavyotumia kupata taarifa hasa mitandao ya kijamii pia
wafuate maadili ya uandishi wa habari na kuandika habari kutoka kwenye
vyanzo vya uhakika visivyo na shaka.
Aidha CUF
imetoa angalizo kwa wanachama wake wote kuwa makini na taarifa
wanazopokea na wazithibitishe kwa umakini ili kuwa na uhakika na kuepuka
kupotoshwa.
chanzo: Millardayo.com
No comments
+255716829257