CHILE WATINGA ROBO FAINALI MICHUANO YA COPA AMERICA..
Wachezaji Eduardo Vargas na Alexis Sanchez wameifungia bao mbili kila mmoja na kuwahakikishia mabingwa watetezi Chile nafasi ya Robo kutoka Kundi D katika michuano ya Copa America.
Chile wamemaliza Nafasi ya Pili kwenye Kundi D wakiwa nyuma ya Argentina ambao wameichapa Bolivia 3-0 kwa Bao za Kipindi cha Kwanza za Erick Lamela, Ezequiel Lavezzi na Victor Cuesta.
Bao za Panama ambao pia walikuwa na matumaini ya kufuzu zilifungwa na Miguel Camargo na Abdiel Arroyo.
Kwenye Robo Fainali, Chile watacheza na Mexico na Argentina kuivaa Venecuela, kesho Ijumaa 17 Juni Marekani itachuana na Ecuador .
Mashindano haya Copa América Centenario ni mahsusi kusheherekea Miaka 100 ya Copa America, Mashindano ya Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kusini, CONMEBOL, ambayo yalianzishwa Mwaka 1916.
Hii ni mara ya kwanza kwa michuano hii kuchezwa nje ya Marekani ya Kusini.
Haya yatakuwa ni Mashindano ya 45 kufanyika na kawaida yake hufanyika kila baada ya Miaka Minne lakini safari hii CONMEBOL na CONCACAF, Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kaskazini, Kati na Nchi za Visiwa vya Caribbean, walikubaliana kuandaa Mashindano maalum.
Safari hii michuano hii itakuwa na Nchi 16, badala ya 12 za kawaida, kwa kushirikisha Nchi 10 kutoka CONMEBOL na 6 za CONCACAF.
Kawaida Mshindi wa Copa America huiwakilisha Marekani ya Kusini kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho lakini Mshindi wa Copa América Centenario hatapewa hilo kwani Mwaka Jana Chile, wakiwa Nyumbani kwao, ndio walitwaa Copa America ya kawaida na wao ndio watashiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho Mwakani, 2017, huko Urusi .
chanzo: BBC
No comments
+255716829257