MFAHAMU SITI BINTI SAAD MALAIKA WA PWANI YA AFRIKA MASHARIKI..
Siti binti Saad ni
nani?
Kwa wanao ifahamu vizuri historia ya pwani ya Afrika mashariki,
Siti binti Saad ni mwanamke maarufu sana huko visiwani Zanzibar, alizaliwa
mwaka 1880 katika kijiji cha Fumba visiwani humo, baba yake alikuwa mnyamwezi
kutoka Tabora na mama yake alikuwa mzigua kutoka Tanga.Alikulia katika familia
ya hali duni sana, baba na mama yake walijishughulisha na shughuli za kilimo na
ufinyanzi.
Alipatiwa jina la
“siti” na waarabu lenye maana ya “mtumwa” kwakua alizaliwa katika kipindi cha
biashara ya utumwa katika pwani ya Afrika mashariki katika miaka ya mwanzo ya
karne ya 20.
Siti alijaliwa kipaji
cha kuimba na sauti tamu ya kumtoa nyoka pangoni aliyoitumia vyema kuzinadi
bidhaa zilizofinyangwa na mama yake ili kujikimu na hali ngumu ya maisha katika
kipindi hicho cha utumwa wa waarabu visiwani Zanzibar.
Siti alijipatia
umaarufu zaidi baada ya kuhamia mjini kutafuta maisha ambako alijihusisha na
uimbaji wa nyimbo za taarabu zenye ujumbe mzito ikiwemo kupigania uhuru ili
kikomesha biashara ya utumwa katika
pwani ya Afrika mashariki.
“..siti binti saadi kawa mtu lini,
Kaja na kaniki duni
Kama si sauti angekula nini..”
Ushujaa na uzalendo wa Siti uliwasisimua wengi wakiwemo waandishi
mashuhuru wa vitabu waliotumia kazi zao kuelezea umaarufu wa mwanamke huyu
shujaa wa Afrika.Shabani Robert katika kitabu chake “WASIFU WA SITI BINTI SAAD”
alitumia ufundi wa hali ya juu kufafanua jinsi Siti alivyokua shujaa mwenye
kipaji na utashi mkubwa.
No comments
+255716829257