Habari mpya

IBRA DA HUSTLER AELEKEZA HISIA ZAKE KWA MWANADADA JOKATE KIDOTI...

 
Aliyekuwa miongoni mwa Rapperz waliokuwa wakiliunda kundi la Nako2nako kutoka JIJINI Arusha, Ibra Da Hustler amefunguka ya moyoni juu ya msichana anayempenda miongoni mwa warembo wa kitanzania wanaitingisha bongo land kwa uzuri wa asili waliojaliwa na mungu.
Akiongea na Jembe FM katika mahojiano maalumu, Da Hustler amesema mwanadada Jokate Mwegelo a.k.a Kidoti ndiye mwanamke pekee anayeichanganya akili yake na anatamani sana angekuwa naye katika mahusiano.
Alitiririka hivi..“Choice yangu mimi kama kudate na kastaa ka Bongo katakuwa kale kabinti kanachoitwa Jokate Mwegelo, she is fly meeen, I like her height, she got nice lips, she is so cute,” Ibrah alimuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Napenda smile yake, napenda style yake, napenda kila kitu chake, jinsi anavyoongea, anavyotembea, she is so high above the sea level, true say, no lie, mtoto mkali sana yaani,” aliongeza.
Ibra Da Hustler anafanya vizuri na wimbo wake mpya "lets go" aliomshirikisha G.Nako.

No comments

+255716829257