Habari mpya

PERUZI HABARI KUU ZA ULIMWENGU LEO AGOSTI 4..

 1. Mwenge wa Olimpiki wawasili Rio
 Mwenge wa Olimpiki
Mwenge wa Olimpiki umewasili mjini Rio de Janeiro kwa njia mashua baada ya safari ya miezi mitatu ukitembea kwenye miji ya Brazil.
Meya wa Rio alibeba mwenge huo katika safari yake ya mwisho.
Lakini zilishuhudiwa ghasia wakati safari ya mwenge ilitatizwa na mamia ya waandamanaji wanaolalamikia gharama kubwa ya kundaa mashindano hayo.
Polisi wa kupambana na ghasia walitumia gesi ya kutoa machozi kutawanya umati.
Brazil inakumbwa na hali mbaya ya uchumi na mzozo wa kisiasa huku maandamano zaidi yakitarajiwa kabla ya sherehe za ufunguzi siku ya Ijumaa.

2. Mwanamke auawa kwa kudungwa kisu London

 Mwanamke
Mwanamke moja ameuawa na hadi watu watano kujeruhiwa kwenye shambulizi la kutumia kisu mjini London, Uingereza. Polisi walimkamata mwanamme moja katika eneo hilo.
Polisi wanasema kuwa ugaidi ni moja ya masuala yanayofanyiwa uchunguzi.
Siku ya Jumatano mamia zaidi ya polisi walianza kupiga doria katika mitaa ya mji wa London.

3. Trump asema bado kuna umoja kambi yake

 Donald Trump
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini marekani Donald Trump amesisitiza kuwa kampeni yake ina umoja licha ya madai kuibuka madai kuwa kuna tofauti ndani ya uingozi wa chama.
Wakati wa mkutano mjini Florida Trump alisema kuwa chama hicho kina umoja kuliko siku zilizopita.
Lakini kama moja ya dalili ya kuwepo mgawanyiko ndani ya chama, spika wa zamani wa bunge Newt Gingrich, ambaye ni mfuasi wa Trump alisema kuwa mgombea huyo anamsadia Hillary Clinton kushinda kwa kuonyesha kuwa hakubaliki zaidi kuliko Hillary.

4. Uchunguzi Canada kuhusu kutoweka kwa wanawake

 Watetezi wa wanawake
Canada imeanzisha uchunguaia kuhusu kuuawa na kutoweka kwa wanawake na wasichana wa jamii asili.
Suala amabalo limesababisha shutuma za kimataifa.
Zaidi ya wanawake na wasichana wa asili wapatao 1,200 wametoweka au kuuawa tangu mwaka 1980 suala ambalo serikali ya awali ya kihafidhina inasema limetokana na ghasia za kinyumbani.
Serikli ya sasa inasema kuwa kuna matatizo yanayohusina na ubaguzi, umaskini na ukoloni yanayohitaji kuchunguzwa. Inasema kuwa uchunguzi ni hatua muhumu ya kuleta uwiano kati ya Canada na watu wake wa asili.

No comments

+255716829257