Habari mpya

SASA LEROY SANE ANAJONGEA MANCHESTER CITY..

 
Leroy Sane anakaribia kumaliza uhamisho wake katika klabu ya Manchester City kutoka Schalke kwa kitita cha pauni milioni 37.
Klabu hiyo ya Bundesliga ilitangaza siku ya Jumatatu kwamba kiungo huyo wa kati hakujiunga na City wakati wa mazoezi yao huko Austria kabla ya kuanza kwa msimu ujao na kwamba alisalia Manchester.
Mkufunzi wa klabu ya Man City Pep Guardiola alithibitisha mnamo tarehe 21 mwezi Julai kwamba alitaka kumsajili Sane.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 aliisaidia Ujerumani kufika nusu fainali za Euro2016,baada ya kucheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mnamo mwezi Novemba.
Alimwambia kkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo Christian Heidel kwamba alitaka kuondoka katika klabu hiyo.

No comments

+255716829257