Habari mpya

Bale, Griezmann na Ronaldo kuwania tuzo ya mchezaji bora wa UEFA..

Shirikisho la Soka Barani Ulaya UEFA, limetoa rasmi majina ya wachezaji walioingia kwenye hatua ya mwisho ya kuwania tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya mwaka huu.
B3
Wachezaji walioingia kwenye tatu bora ya mwaka huu ni Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Gareth Bale (Real Madrid) na Cristiano Ronaldo (Real Madrid).
Hii ni orodha ya wachezaji waliofanikiwa kuingia kwenye kumi bora; Luis Suárez (Barcelona), Lionel Messi (Barcelona), Gianluigi Buffon (Juventus), Pepe (Real Madrid), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Manuel Neuer (Bayern München), Gareth Bale (Real Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Thomas Müller (Bayern München).
UE
Tuzo hiyo itatolewa mjini Monaco mwezi August 25.
chanzo: Bongo5

No comments

+255716829257