Habari mpya

Joh Makini aeleza alivyojipanga kufanya video ya collabo yake na Davido..

Nimebahatika kusikiliza collabo ya Joh Makini na staa wa Nigeria, Davido, na ninasema kwa kujiamini kuwa ngoma hiyo itasumbua sana ikitoka.
Joh
Lakini Joh amesema hawezi akautoa wimbo huo bila video yake na upatikanaji wa Davido tangu asaini na Sony Music si mrahisi tena kama zamani.
“Mshkaji yuko busy sana, hata kama unamfollow kwenye social networks, ni mtu ambaye anafanya tour nchi nyingi, yuko studio halafu yupo Nigeria,” Joh ameiambia Bongo5.
“Taratibu za video usema ukweli inabidi nikae chini niangalie timing na nicheck kwanza ratiba yake kwasababu obvious nitataka kufanya na Campos hiyo ni South Africa, na wakati Davido yupo kwenye biashara zake huwezi kusimamisha ratiba yake nyingine ukamwambia aje SA kurekodi, halafu unajua ni mtu anayesafiri na watu wengi, yaani kumsafirisha tu yeye ni gharama kubwa kitu ambacho nitakuwa muongo nikisema naweza kumtia kwenye private jet sasa hivi,” ameongeza.
Mwamba huyo wa Kaskazini anasema anaangalia muda muafaka kwa Davido hasa kama akiwa SA kwa shughuli zake binafsi na kutumia wasaa huo kumkamata na kufanya video yao.
Joh kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Perfect Combo’ aliyomshirikisha msanii mwingine wa Nigeria, Chidinma.
Tazama video hapa chini..

No comments

+255716829257