Habari mpya

TEKNOLOJIA: JUNO YATUMA PICHA YA KWANZA YA SAYARI YA JUPITER..

JupiterChombo cha anga za juu cha shirika la Marekani la NASA kilichopewa jina Juno kimetuma picha za kwanza za sayari ya Jupiter.
Moja ya hizo, iliyotolewa na NASA Jumanne inaonesha sayari hiyo ikiwa imezungukwa na miezi mitatu kati ya miezi yake minne mikubwa.
Miezi inayoonekana ni Lo, Europa na Ganymede. Mwezi huo mwingine uitwao Callisto hauonekani.
Picha hiyo ilipigwa Jumamosi sayari Juno ilipokuwa inazunguka sayari hiyo ikiwa umbali wa maili milioni tatu.
Hata katika umbali huo, Shimo Jekundu, lililosababishwa na dhoruba kali kwenye sayari hiyo karne nyingi zilizopita, linaonekana.


JunoImage copyrightGETTY
Image captionWataalamu wa Nasa wakisherehekea kufika kwa Juno mzingo wa Jupiter

Juno iliingia katika mzingo wa Jupiter wiki iliyopita na kuanza kuizunguka sayari hiyo ambalo pia hufahamika kama Zohali au Zozali.
Safari yake kutoka duniani hadi ilichukua miaka mitano.
Juno itachunguza na kupeleleza sayari hiyo kwa miezi 20, lengo kuu likiwa kusaidia wanasayansi kubaini asili ya sayari hiyo ambayo wanaamini inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi asili ya mfumo wa jua.
Chombo hicho cha juu kilipokuwa kinaikaribia Jupiter, kamera zake na mitambo mingine muhimu vilizimwa kuzuia visiharibiwe na miali nururishi. Baadaye, vilifunguliwa.


JunoImage copyrightAFP
Image captionPicha za karibu zaidi za Jupiter zinatarajiwa mwezi ujao

Wanasayansi wanatarajia picha za karibu zaidi za Jupiter zitapokelewa mwezi ujao.
  • Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara 300 zaidi
  • Sayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja huko hudumu saa 10.
  • Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.
  • Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018
  • CHANZO: BBC

No comments

+255716829257