JE UNA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI?? JIFUNZE HAYA..
Tatizo la kukosa usingizi huenda
likawa ishara ya kutambua mapema maradhi ya kusahau au ''Alzheimer'' kwa mujibu
wa utafiti uliofanywa kwa kutumia panya ambaye ana maumbile yanayofananishwa na
binadamu.
Vipande vya protini, kwa lugha ya
kitaalamu (plaques) au uchafu kwenye ubongo yanadhaniwa kuwa sehemu nyeti
inayosababisha maradhi haya.
Taarifa zinazohusianaafyaUtafiti
uliofanywa na kuchapishwa katika jarida la tafsiri ya matukio ya Sayansi,
umeonyesha kuwa punde chembe chembe za uchafu ule ulipoanza kukua kwenye ubongo
wa panya, usingizi ukaanza kuwa tatizo kwa viumbe hao.
Taasisi inayosimamia utafiti wa
maradhi hayo, (Alzheimer's Research UK) imehimiza kuwa ikiwa uhusiano huo
unaweza kuthibitishwa huenda ikawa muhimu kwa Madaktari.
Utafiti wa kutaka kugundua mapema
kama mtu anaelekea kukumbwa na maradhi ya Alzheimer inadhaniwa kuwa muhimu
katika kutibu maradhi hayo.
Wagonjwa hawaonyeshi dalili kupitia
hisia au kumbukumbu zao hadi baada ya mda mrefu wa maradhi kumkumba mgonjwa.
Yanapofikia hapa sehemu za ubongo huwa zimeharibika kiasi kwamba tiba inakua
vigumu kupatikana au hata kushindwa kupatikana.
Ndiyo sababu wataalamu wanafanya
juhudi za kuanza mapema kugundua kama mtu atapata maradhi haya, miaka kadhaa
kabla ya dalili hizo kujitokeza.
Viwango vya protini ijulikanayo
kama Beta Amyloid kimaumbile hupanda na kushuka miongoni mwa binadamu na pia
panya katika kipindi cha saa 24. Hata hivyo ni ile protini ambayo hujenga
uchafu usiofutika kwenye ubongo na maradhi ya Alzheimer.
Majaribio yaliyofanywa katika Chuo
Kikuu cha Washington yameonyesha kuwa panya wanaotoka usiku kwa kawaida hulala
kwa dakika 40 kwa kila saa mchana. Lakini ubongo ulipoanza kupatwa na uchafu
panya hawa wakaanza kusinzia kwa dakika 30 pekee.Mmojapo wa wataalamu, Prof
David Holtzman, alisema: "endapo mapungufu katika usingizi huanza mapema
kiasi hiki katika ugonjwa wa Alzheimer, mabadiliko hayo yanaweza kutupa ishara
ya wepesi wa kuweza kuyatambua maradhi haya."
"ikiwa matatizo haya ya
usingizi yapo, hatuelewi hasa yanachukua mfumo gani, kupungua kwa usingizi
kikamilifu au ni tatizo la kushindwa kabisa kulala au ni kitu tofauti
kabisa."
Hata hivyo, utafiti unaofanyika kwa
kutumia panya mara nyingi hayafai kutumika kwa binadamu kwa sababu nyingi
zinazosababisha kutatizika na usingizi.
Dr Marie Janson, kutoka shirika la
kujitolea Alzheimer's Research UK, ametaka utafiti zaidi ufanywe kwa kuwapima
binadamu kuona kama kuna uhusiano baina ya matatizo ya kukosa usingizi na
ugonjwa wa Alzheimer.
Aliongezea kuwa: "tayari
umekuwepo utafiti unaounganisha mabadiliko katika usingizi huchangia katika
matumizi ya ubongo kwa fikra, lakini matokeo haya yanaonyesha kuwa kuna
uwezekano wa kuwa mapungufu katika usingizi pia inaweza kuwa ishara na onyo la
maradhi ya kusahau au Alzheimer.
No comments
+255716829257