JIFUNZA MENGI KUHUSU UGONJWA WA SARATANI YA MATITI KWA WANAWAKE..
Saratani
ya matiti ni vikundi vya seli za kansa ambavyo huanza kwenye seli za matiti.
Vikundi hivyo vya seli za kansa ni chembechembe za saratani ambavyo huweza
kukua na kuvamia tishu za karibu au kuenea maeneo ya mbali mbali ya
mwili. Ugonjwa huu huwakumba wanawake lakini pia wanaume wanaweza kupata.
Kwa
mujibu wa Shirika la Afya Duniani, kansa ya matiti ni kansa ambayo maranyingi
huathiri wanawake wengi duniani kote, maisha ya mamia ya maelfu ya wanawake
kila mwaka huathiri nchi katika ngazi zote za maisha ya kisasa.
CHANZO
CHA UGONJWA
Ukiambiwa
kwamba una saratani ya matiti, ni jambo la kawaida kustajabu nini inaweza kuwa
sababu ya wewe kupata ugonjwa huo. Lakini hakuna anaejua chanzo na sababu
halisi ya kansa ya matiti. Madaktari mara chache hujua kwa nini mwanamke mmoja
anaweza kuwa na saratani ya matiti na mwingine hana, na wanawake wengi ambao
wana kansa ya matiti kamwe huwa hawana uwezo wa chanzo halisi cha ugonjwa huo.
Tunachojua ni kwamba kansa ya matiti daima husababishwa na uharibifu wa
vinasaba(DNA) vya seli.
DALILI
ZA UGONJWA
Katika
hatua za kwanza za ugonjwa, kansa ya matiti hua haina dalili zozote. Lakini
saratani ikishaanza kukomaa unaweza kutambua dalili zifuatazo;
- Uvimbe
kwenye mbavu karibia kwenye titi
- Maumivu
ya matiti. Ingawa kwa kawaida Uvimbe husababisha maumivu, Maumivu yanaweza
kuwa ni ishara ya saratani ya matiti.
- Kuhisi
kama kuna vitu vilivyotambaa juu ya matiti, ambavyo huwa ni ishara ya
uvimbe.
- Mabadiliko
yoyote kuhusu ukubwa, joto, ugumu au ulaini wa matiti. Pia ukiona sehemu
ndogo ya titi iliyo Nyekundu sana au kama ngozi ya machungwa inaweza kuwa
ni ishara ya saratani ya matiti iliyokomaa.
- Mabadiliko
kwenye chuchu, kama vile Chuchu kujivuta kwa ndani, kuwa na dimpo(kama
vishimo), kuwasha, kuhisi kuungua au vidonda. Magamba kama upele kwenye
chuchu ni dalili ya ugonjwa unaoitwa Paget(kwa lugha ya kimombo), ambao
unaweza kuhusishwa na saratani ya matiti.
- Kutokwa
na majimaji kwenye chuchu yanayoweza kuwa meupe kabisa, yenye damu, au
rangi nyingine.
- Kuwa
na kama vijiwe chini ya ngozi ya titi.
- Muonekano
wa eneo fulani la titi kuwa tofauti kabisa na maeneo mengine ya titi.
**Mara
uonapo dalili zilizotajwa hapo juu fika Hosipitali kwa uhunguzi zaidi
TIBA
YA UGONJWA
Matibabu
ya saratani ya matitini yamezidi kuboreshwa siku hadi siku, na kwa sasa watu
wamekuwa na njia nyingi za kutibu saratani hii kuliko hapo kabla. kuwa na njia
nyingi za kutibu ugonjwa huu, ni fursa nzuri kujifunza mengi na kuchagua njia
gani itakayokufaa kutibu ugonjwa wako.
Haijarishi
umechagua njia gani kutibu ugonjwa huu, kila matibabu ya saratani ya matiti
yana malengo makuu mawili
- kuuondolea
mwili tatizo la kansa kadri iwezekanavyo
- kuzuia
ugonjwa huo kujirudia tena
*Utajuaje
tiba sahihi itakayofaa ugonjwa wako?
Daktari
wako atafikiri juu ya mambo kadhaa kabla ya yeye kupendekeza matibabu sahihi ya
ugonjwa wako. Kwa mfano kwa kuangalia mambo yafuatayo;
- Aina
ya saratani ya matiti uliyonayo
- Ukubwa
wa saratani yako na jinsi ilivyoenea mwilini mwako
- Kama
saratani yako ina vitu viitwavyo 'receptors' kwa protini aina ya
HER2 , estrogen, na progesterone, au vitu vingine.
- Umri
wako, kama wewe umefikia umri wa kutopata hedhi, masharti mengine ya afya,
na matakwa yako binafsi ni mambo mengine ambayo husaidia kutoa maamuzi
sahihi ya tiba yako.
*Aina
Mbalimbali za Kutibu Ugonjwa huu.
Baadhi
ya matibabu huondoa au kuharibu ugonjwa ndani ya matiti na tishu za jirani,
kama vile tezi(lymph nodes). Matibabu hayo ni pamoja na;
- Upasuaji
wa kuondoa titi zima, uitwao "mastectomy", au kuondoa tu uvimbe
na tishu za karibu yake, uitwao "lumpectomy" au upasuaji wa
kuhifadhi matiti. Kuna aina mbalimbali za tiba hizi mbili.
- Tiba
ya mionzi, ambayo hutumia mawimbi ya nishati ya juu(mionzi)kuua seli za
saratani. Tiba ya mionzi hutibu saratani kwa kutumia mawimbi ya
nishati ya juu(mionzi) kuua seli zenye kansa. Lengo ni kuharibu kansa bila
kuumiza seli zingine zenye afya. Tiba hii inaweza kusababisha
madhara, lakini ina utofauti kwa kila mtu. Madhara utakayopata hutegemea
aina ya mionzi utakayopata, kiwango cha ugonjwa, sehemu ya mwili wako
itakayopata matibabu, na afya yako kwa ujumla.
Matibabu
mengine huharibu au kudhibiti chembechembe za saratani mwili mzima. Matibabu
hayo ni kama yafuatayo
- Kutumia
madawa (Chemotherapy) kuua seli za saratani. Kadiri hizi dawa zinavyokua
na nguvu zaidi ya kupambana na magonjwa, ndivyo jinsi zinavyoweza
kusababisha madhara, kama kichefuchefu, kupoteza nywele, hedhi kukoma
mapema kabla ya umri, na uchovu.
- Tiba
ya homoni inatumia madawa ya kuzuia homoni, hasa estrogen, ambazo
huchochea ukuaji wa chembechembe za saratani ya matiti. Madawa hayo ni
pamoja na tamoxifen (Nolvadex, Soltamox) kwa wanawake kabla na baada ya
kukoma kwa hedhi, anastrozole (Arimidex), exemestane (Aromasin), na
letrozole (Femara) kwa wanawake wanaokaribia ukomo wa hedhi zao. Madhara
ya madawa haya ni pamoja na kuwa na joto kali ikiambatana na mapigo ya
moyo ya kasi pamoja na Uke kukauka au kuwa Mkavu. Baadhi ya aina hizi za
tiba hufanya kazi kuzuia ovari kutotoa homoni, aidha kwa njia ya upasuaji
au kutumia madawa.
- Matibabu
yanayolengwa ni hutumia madwa kama vile lapatinib (Tykerb), pertuzumab
(Perjeta), na trastuzumab (Herceptin). Dawa hizi husababisha kinga ya
mwili kuharibu kansa. pia hulenga seli za kansa ya matiti ambazo zina
kiwango kikubwa cha protini inayoitwa HER2.
- Palbociclib
(Ibrance) hufanya kazi za kuzuia molekuli ambazo hukuza ukuaji wa kansa.
Pamoja na letrozole, palbociclib ni kwa wanawake wanaokaribia ukomo wa
hedhi zao na pia huwa na aina fulani ya kansa iliyokomaa.
Unaweza
kupata tiba ya dawa, tiba ya homoni, au tiba yoyote inayohusika na upasuaji au
mionzi. Tiba hizi huua seli zote za kansa zilizoachwa au kushindwa kutibiwa na
matibabu mengine.
NAMNA
YA KUEPUKA UGONJWA HUU
Mabadiliko
ya mwenendo wa maisha yanaonyesha kupunguza hatari ya kupata kansa ya matiti.
Zifuatazo ni hatua unazoweza kuchukua ili kupunguza hatari ya kupata ugonjwa
huu
- Punguza
matumizi ya Pombe.
Jinsi unavyoendelea kunywa pombe, ndivyo jinsi unavyokua na hatari kubwa
zaidi ya kupata kansa ya matiti. kulingana na utafiti juu ya athari za
pombe kusababisha hatari ya kupata saratani ya matiti inashauriwa kwamba
jitahidi kunywa si zaidi ya chupa 1 ya pombe kwa siku hata hivyo kiasi
kidogo tu huongeza hatari hatari ya kupata ugonjwa huu.
- Usivute
sigara.
ushahidi wa kitafiti unaonyesha uhusiano kati ya sigara na hatari ya
saratani ya matiti, hasa kwa wanawake ambao hawajafikia ukomo wa hedhi
zao. Aidha, kutovuta sigara ni njia moja wapo ya kuboresha afya yako kwa
ujumla.
- Dhibiti
uzito wako.
Kuwa na uzito mkubwa kunaongeza hatari ya kupata kansa ya matiti. Hii ina
ukweli hasa kama unene kupita kiasi unapotokea baadaye katika maisha, hasa
baada ya ukomo wa hedhi.
- Fanya
Mazoezi ya viungo.
Shughuli za kimwili zinaweza kukusaidia kudumisha afya na kupunguza uzito
hatimaye kupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti. Kwa watu wazima
zaidi na afya, watafiti wanapendekeza angalau muhusika afanye mazoezi au
shughuli yoyote ya kutoa jasho kwa dakika 150 or dakika 75 kwa mazoezi
makari ya viungo kila wiki kwa wiki.
- Nyonyesha. Kunyonyesha kunaweza kuwa na
jukumu kubwa katika kuzuia kansa ya matiti. wanawake waliozaa wanapaswa
kunyonyesha sana kadri wawezavyo, Kadri unavyonyonyesha ndivyo jinsi
unavyojiongezea kinga ya kutopata ugonjwa huu.
- Zuia
dozi na muda wa tiba ya homoni (Hormotherapy). Mchanganyiko wa homoni tiba
kwa zaidi ya miaka 3-5 huoneza hatari ya kupata saratani ya matiti. Kama
wewe unatumia homoni tiba kwa dalili zinazohusu wanawake wenye ukomo wa
hedhi, muulize daktari wako kuhusu njia zingine za tiba. Unaweza kuwa na
uwezo wa kusimamia dalili zako kwa kutumia tiba zisizotumia homoni
(nonhormonal) na dawa mbalimbali.
- Epuka
kuwa karibu na mionzi na uchafuzi wa mazingira. kama vile 'computerized
tomography', hutumia viwango vya juu vya mionzi. Baadhi ya tafiti
zinaonyesha uhusiano kati ya saratani ya matiti na mionzi. Jitahidi
kutoikaribia mionzi na uchafuzi wa mazingira kama maeneo ya viwanda.
CREDIT: Mjasiriamali hodari
No comments
+255716829257