CAF: MAMELODI SUNDOWNS WAITANDIKA ENYIMBA 2-1..
Klabu ya soka ya Mamelodi Sundowns
ya Afrika kusini imeichabanga Enyimba ya Nigeria mabao 2-1 mjini
Pretoria katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika siku moja baada
ya vigogo wengine wa Afrika Al Ahly kuambulia kichapo nyumbani dhidi ya
Asec Mimosas.
Kabla ya mchezo huo Sundowns waliwafunga Entente
Setif ya Algeria 2-0 lakini mchezo huo ukatangazwa batili baada ya Setif
kushindwa kuwazuia mashabiki wao kufanya fujo.Ushindi huo unaipa Sundowns alama sawa na Zamalek katika kundi B timu zote zikiwa na ushindi wa mchezo mmoja huku zikiwa zimesalia timu tatu katika kundi hilo.
Enyimba wanaburuza mkia wakiwa bado hawajapata alama yoyote katika michezo yao ya ufunguzi.
No comments
+255716829257