Habari mpya

Yamoto Band kuachia albamu yao ya kwanza

YAMOTO
Bendi ya muziki Yamoto Band, baada ya kufanya vizuri na kazi zao nyingi, inatarajia kuachia albamu yake ya kwanza hivi karibubuni.
YAMOTO
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Mkurugenzi wa Yamoto Band, Said Fella amesema mpango wa ujio wa albamu hiyo umekamilika.
“Kusema kweli albamu ipo tayari, sema tulikuwa kwenye mgongano kuhusu kulipa vati ya TRA ya asilimia 18, kwa sababu wasambazaji walikuwa wanataka tulipe sisi 18% yote, lakini tukawaambia tunatakiwa tugawane, kwa hiyo ndo tupo kwenye mazungumzo ya mwisho,” alisema Fella.
Aliongeza, “Nadhani haya mazungumzo yakikamilika, tutawatangazia mashabiki rasmi, itapatikana wapi na bei zake, kalini wajue albamu ipo tayari,
chanzo: bongo5

No comments

+255716829257