Chibwa kuachia ngoma mpya na Elephant Man April 29
Msanii wa mziki wa Dance Hall hapa bongo Chibwa baada ya ukimya wa muda kiasi, ameamua kuzidi kufanya collaboration na wasanii wa kimataifa kama Been Man na Elephant Man.
Chibwa amesema anatarajia kuachia ngoma na Elephant Man tarehe 29 mwezi huu, huku akiwataka mashabiki wa mziki wake Tanzania kukaa tayari ,kupokea wimbo huo ambao mwenyewe anadai kujiandaa vyema zaidi kuliko ngoma zake zote
Akiongea na eNewz ya eatv.tv kuhusiana na kilichokuwa kinamzuia yeye kufanya collabo tangu kitambo kama alivyokuwa akiahidi hapo awali kuwa angefanya collabo na Been Man.
Chibwa amesema kwamba suala la menejimenti ndilo lililokuwa likisababisha yeye kushindwa kufanya collabo na wasanii wa nje kwani hapo awali hakuwa na mtu wa kumdhamini, lakini kwa sasa alipopata udhamini kutoka kwa Zanmounten mambo mengi yamekuwa rahisi kufanyika
Hata hivyo Chibwa amefunguka kuwa siku si nyingi atafata nyendo za Roma, kwa kufunga pingu za maisha na mwanamke ambaye ameishi naye mda bila kufunga ndoa na kwa sasa wana mtoto.
chanzo: bongo5
No comments
+255716829257