Uadilifu wa rais mpya wa Fifa watiliwa Shaka
Rais mpya wa shirikisho la soka duniani Fifa,Gianni Infantino alisaini kandarasi na wafanyibiashara wawili ambao wanatuhumiwa na kutoa hongo,kulingana na stakhabadhi zilizofichuliwa.
Hugo na Mariano Jinkis walinunua haki za maonyesho ya moja kwa moja ya mechi za kombe la vilabu bingwa runingani na kuziuza mara tatu ya bei waliyonunua.
Kandarasi hiyo ya mwaka 2006 ilitiwa saini na Infantino alipokuwa mkurugenzi wa Uefa.
Ni miongoni mwa stakhabadhi milioni 11 zilizofichuliwa katika kampuni ya mawakili nchini Panama Mossack Fonseca.
Awali Uefa ilikana kufanya biashara na mtu yeyote miongoni mwa watu 14 walioshtakiwa na shirika la FBI katika uchunguzi wake wa ufisadi katika soka duniani.
Sasa imeambia BBC kwamba haki za runinga ziliuzwa kwa mtu aliyezitaka haki hizo kwa kiwango cha juu katika zabuni iliofanywa kwa uwazi.
Duru kutoka kwa afisa mkuu wa Fifa ambaye jina lake halikutajwa zimeambia BBC kwamba zabuni hiyo lazima ichunguzwe na kamati ya maadili ya Fifa kwa maslahi ya uwazi.
Infantino ambaye alichaguliwa rais wa shirikisho la Fifa tarehe 26 mwezi Februari ametoa taarifa akisema kuwa anasikitika kwamba uadilfu wake unatiliwa shaka.
CHANZO:BBC
No comments
+255716829257