ICC: Ruto na Sang hawana kesi ya kujibu
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imeamua Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto hana kesi ya kujibu kuhusiana na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyokuwa yanamkabili.
Aidha, imeamua pia kwamba mwanahabari Joshua arap Sang, aliyeshtakiwa pamoja na Bw Ruto, hana kesi ya kujibu.
Bw Ruto alikabiliwa na mashtaka ya mauaji, kuhamisha watu kwa lazima na mateso yaliyotekelezwa wakati wa vita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Alikana mashtaka hayo na mawakili wake walitaka kesi hiyo itupiliwe mbali kutokana na ukosefu wa ushahidi.
Watu takriban 1,200 waliuawa wakati wa mapigano hayo.
Majaji wamesema upande wa mashtaka haukutoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai dhidi ya Bw Ruto na Bw Sang.
- Ruto ashinda rufaa mahakama ya ICC
- Mashahidi wa Ruto katika ICC
- Bensouda:Sikabiliwi na shinikizo zozote
Desemba mwaka 2014, mwendesha mashtaka aliondoa mashtaka sawa dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta akisema mashahidi walikuwa wametishiwa na kubadilisha ushahidi wao.
Bw Ruto na Bw Kenyatta walikuwa kwenye mirengo pinzani wakati wa uchaguzi wa 2007 lakini waliunda muungano wa kisiasa na wakashinda uchaguzi mkuu wa 2013.
No comments
+255716829257