Habari mpya

URA YASHINDA KOMBE LA MAPINDUZI.

ura
Klabu ya URA ya Uganda (pichani) imefanikiwa kushinda Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Mtibwa Sugar magoli 3 kwa 1 katika mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Amaan uliopo visiwani Zanzibar.
Magoli ya URL katika ushindi huo yalifungwa na Julias Ntambi na Peter Lwasa aliyefunga magoli mawili huku goli la kufutia machozi la Mtibwa likifungwa na Jaffar Salum.
Baada ya ushindi huo URL imefanikiwa kushinda kikombe na zawadi ya Milioni 10 kutoka kwa waandaji wa mashindano hayo na inakuwa ni timu ya pili kutokea Uganda kushinda kombe hilo baada ya KCCA kufanya hivyo mwaka 2014.
Mtibwa nayo imefanikiwa kupata kitita cha Milioni 5 na sasa inajiandaa kurejea Tanzania bara kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu iliyopo mbele yao.

No comments

+255716829257