Habari mpya

MBWANA SAMATTA AZAWADIWA

Samatta


Image captionSamatta aliibuka mfungaji mabao bora ligi ya klabu bingwa Afrika 2015

Mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa nyumbani Mbwana Samatta amekabidhiwa sehemu ya ardhi na serikali ya Tanzania kufuatia uhodari wake uliomwezesha kuondoka na tuzo hiyo na kuisaidia TP Mazembe kutwaa kombe la vilabu bingwa Afrika.
Mchezaji huyo pia alitunukiwa zawadi nyinginezo kwenye hafla iliyoandaliwa ili kusherekea mafanikio yake katika soka yaliyoiweka Tanzania katika ramani ya soka.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wadau wa michezo nchini Tazania wakiwemo waziri wa michezo Nape Nnauye na Thomas Ulimwengu ambaye ni mchezaji mwenza wa Samatta.
Amepewa kipande cha ardhi eneo la Kigamboni, Dar es Salaam na serikali kupitia wizara ya ardhi na nyumba.
Mchezaji huyo pia ameteuliwa nahodha mpya wa timu ya taifa Taifa Stars, nafasi ambayo awali ilishikiliwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anayeichezea klabu ya Yanga, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.
Samatta, maarufu ‘Samagoal’ aliwapiku Robert Kadiaba na Bounedjah Baghdad wa Algeria anayeichezea klabu ya Etoile du Sahel na kutwaa tuzo hiyo.
Baada ya kupokea taji lake katika sherehe za kuwatuza wachezaji bora Afrika, mjini Abuja, Samatta alirejea Tanzania na baadaye kualikwa na Rais wa Zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Mnamo mwaka wa 2013, serikali ya Nigeria iliwakabidhi wachezaji wake sehemu ya ardhi mjini Abuja na pesa kwa kushinda kombe la Afcon.

No comments

+255716829257