Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu hiyo imemnunua kiungo wa kati wa FC Basel Mohamed Elneny.
Mchezaji huyo anaweza kuwachezea dhidi ya Stoke Jumapili.
Elneny, 23, anaripotiwa kuwagharimu Gunners £5m na anahitimu kuwachezea katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Akizungumza baada ya Arsenal kutoka sare ya 3-3 na Liverpool uwanjani Anfield, Wenger alisema: "Amejiunga nasi na tutamchunguza kuona iwapo anatosha kucheza Jumapili.”
source: BBC
No comments
+255716829257