TIMU ya Azam FC imetamba kuwa itamaliza machungu yake ya Kombe la Mapinduzi kwa kuifunga African Sports Jumamosi katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Azam FC ambayo kwa sasa inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 35, imesisitiza kuwa ushindi wa kishindo utaifanya izidi kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Msemaji wa Azam FC, Jafar Iddi alisema timu yake haina wasiwasi na ushindi huo na hasa ikizingatiwa wachezaji wake wamepata muda wa kutosha kujiandaa na ligi.
“Sisi kwa sasa tunaongoza ligi tukiwa na pointi 35 na kwa hiyo ni lazima tuhakikishe kuwa tunavuna tena pointi tatu muhimu,” alisema na kuongeza kuwa: “Wachezaji wana hasira na wameahidi burudani safi na naomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kukiona kikosi chao.”
Alisema kwa kuwa timu ilitolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, wachezaji wake wana hasira na michezo ya Ligi Kuu na kuongeza kuwa wamepania ushindi kwa kila timu watakayokutana nayo
No comments
+255716829257