Mdalasini ni viungo vinavyopatikana na kutumika katika chakula na pia hutumika kama dawa. Mdalasini huwa katika hali ya unga au gome la mti. Katika kipindi cha miaka takribani mingi nimekuwa nikitumia mara chache tu kama kiungo cha chakula mpaka nilipoanza safari yangu ya kupunguza uzito. Kwa mara ya kwanza nilipoanza kuitumia nilishangaa kuona mabadiliko mwilini mwangu. Nilijikuta ninakuwa na nguvu ya kutosha siku nzima na pia sikuwa nasikia njaa mara kwa mara kama ilivyo kawaida yangu.
Kuna faida nyingi sana ambazo unaweza kuzipata kwa kutumia mdalasini mara kwa mara hasa wakati wa asubuhi kabla hujala kitu chochote. Kwa wale ambao wana tatizo la sukari kushuka mdalasini unasaidia kuweka sukari katika kiwango kinachoridhisha na hii pia husaidia hata wale ambao wanataka kupunguza uzito. Ni vyema kuhakikisha kuwa kila siku asubuhi unakunywa maji yenye mdalasini na kama utapata na asali au limao itakuwa bora zaidi.
Kwa wale ambao wapo katika safari ya kupunguza uzito mdalasini lazima uwe sehemu ya kiungo katika chai au maji ya kunywa hasa asubuhi. Ni vema kuuhakikisha kuwa unaanza siku yako na kikombe cha mdalasini na asali ukitaka, lakini si muhimu kama huna.
Mdalasini una nafasi kubwa sana katika kuweka sukari katika damu katika kiwango kinachotakiwa na pia kusisimua Enzymes ili kuchochea vichocheo vya mwili kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
Antioxidants katika mdalasini husaidia kuongeza usikivu kwa kukufanya uwe mchangamfu muda mwingi hivyo kutokusikia kuchoka au uvivu usio kuwa na sababu ya msingi. Jaribu kutumia mdalasini uone mafanikio yake ambayo ni kuboresha afya na mwili wako kwa ujumla.
Unaweza pia kupambana na uchovu kwa kutumia mdalasini. Kutumia mdalasini kusaidia insulini katika mwili kufyonza sukari vizuri na kukabiliana na uchovu wako. Kama huwezi kuwa na chai mdalasini kujaribu kuinyunyiza katika vyakula kula kwa faida upeo.
Kutumia mdalasini katika mara kwa mara inaweza kusaidia kuboresha mwili wako kuwa hai wakati wote. Pia huongeza motisha wako, utendaji na kuongeza uchangamfu.
No comments
+255716829257