IRAN YALAANI VIKALI VIKWAZO VIPYA DHIDI YAKE.
Iran imepuuzilia mbali vikwazo vipya dhidi yake ilivyowekewa na Marekani kuhusu mpango wake wa kutengeza makombora.
Vikwazo hivyo havina 'uhalali wa kisheria wala wa kimaadili',msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni amesema.
Mnamo mwezi Oktoba ,Iran ililifanyia jaribio kombora lake lililo na uwezo wa kubeba kichwa cha kombora la nuklia,ikikiuka marufuku ya Umoja wa mataifa.
Hatua hiyo ya Marekani inajiri baada ya vikwazo ilivyowekewa Iran kuondolewa kufuatia mkataba wa mpango wake wa nuklia.
Vikwazo hivyo vipya vitawazuia watu na makampuni 11 wanaohusishwa na mpango huo wa kutengeza makombora kutotumia mfumo wa benki wa Marekani.
Akitangaza hatua hiyo mpya,Adam J Szubin,kaimu katibu wa maswala ya ugaidi nchini Marekani pamoja na maswala ya kiintelijensia kuhusu fedha,amesema kuwa mpango wa kutengeza makombora wa Iran ni tishio kubwa kwa usalama wa kieneo na ulimwengu kwa jumla na kwamba utaendelea kuwekewa vikwazo vya kimataifa.
Hatahivyo msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Iran Hossein Jaber Ansari amesema kwamba mpango huo wa kutengeza makombora haujatengezwa kuwa na malengo ya kubeba silaha za kinuklia.
Source: BBChttp://www.bbc.com/swahili/habari/2016/01/160118_iran-vikwazo-vipya?ocid=socialflow_facebook
No comments
+255716829257