Habari mpya

Almasi kubwa kuliko zote Tanzania yapatikana Shinyanga

Mchimbaji mdogo wa Madini ya Almasi wilaya ya Kishapu ameibuka na Almasi Kubwa kuliko zote zilizowahi kupatikana Tanzania huku Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Bi Zainabu Telack akitoa wito kwa wanunuzi wa Almasi kufika mkoani humo.

Bi. Telack ameitangaza na kuionesha Almasi hiyo mbele ya waandishi wa habari kuwa inauzito wa karati 521 ikiwa ni uzito mkubwa kuliko almasi zote zilizowahi kuchimbwa Mkoani humo na Tanzania kwa ujumla.

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa hadi kufikia sasa  kumekuwa kukichibwa na kupatikana Almasi zenye uzito wa karati 300-421 tu ambazo zimekuwa zikipatikana katika mgodi wa wiliamson- Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

No comments

+255716829257