Papa Francis atoa ujumbe wa amani duniani sikukuu ya Pasaka
Kiongozi wa Kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis ameadhimisha Jumapili ya Pasaka wakati damu ikimwagika nchini Sri Lanka. Papa Francis ameongoza Misa ya wazi katika uwanja wa kanisa la Mtakatifu Petro. Katika sikukuu hii ya Pasaka Wakristo wanasherehekea ufufuo wa Yesu Kristo. Baadaye Papa Francis atatoa hotuba kwa watu wote duniani. Mwaka huu msimu wa Pasaka umekumbwa na uharibifu wa Kanisa la Paris la Notre Dame lililoungua moto wiki iliyopita na mauaji ya watu leo Jumapili huko nchini Sri Lanka. Hapo jana Papa Francis alitoa tahadhari na kuwahimiza watu juu ya umuhimu wa kuacha kukimbilia utajiri na maisha yasiyokuwa na maana kwa kujilimbikizia vitu vinavyokuja na kupita.
No comments
+255716829257