Habari mpya

Rais Magufuli atembelea nyumba za Magomeni, maagizo yatolewa kwa TBA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amewaagiza Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) kuhakikisha mradi wa ujenzi wa nyumba Magomeni unakamilika ifikapo Desemba mwaka huu.
Kwandikwa ameyasema hayo alipofanya ziara katika mradi huo ambao ulizunduliwa rasmi mwaka 2016 na ulitarajiwa kukamilika kwa mwaka mmoja lakini hadi Rais John Magufulialipoutembelea hivi karibuni amekuta bado haujakamilika.
Amesema kuwa kukamilika kwa nyumba hizo kunatarajiwa kuchukua familia 656, hivyo kwa sababu mradi umechelewa Rais Magufuli ametoa msukumo wa kuhakikisha unakamilika kwa wakati kwa sababu unatumia fedha za Watanzania.

No comments

+255716829257