Habari mpya

Hawa aelezea furaha yake baada ya kupata matibabu nchini India

Ipokee hii hapa goodnews kuhusiana na hali ya sasa ya msanii Hawa ambaye yupo nchini India kwaajili ya matibabu ikiwa siku kadhaa zilizopita Manager wa Diamond Platnumz ,Babu Tale aliongelea kuhusiana na hali ya Hawa kupitia ukurasa wake wa instagram.
Kupitia ukurasa wa instagram Babu Tale amepost video ikimuonyesha Hawa akiwa katika hali ya furaha na afya yake ipo vizuri tofauti na mwanzoni na kuwashukuru watanzania kwa maombi ikiwemo kumshukuru Diamond Platnumz kwa msaada alioutoa hadi kufikia hapo alipo.
“Mungu mkubwa hatimae Hawa anatabasamu tena. Acha Leo niamke usiku nisali kwa kumuombea @diamondplatnumzMungu andelee kumfungulia na kumpunguzia mitihani ya kidunia hii iki ulichofanya”
“Hata nikuone umelala ndani ya chupa ya pombe siumii sana sababu naamini unahofu ya Mungu na unaupendo na watu. Basi kuna watu watanipigia wajue Hawa anarudi lini na sinto wajibu😂😂😂 ilaasante @shailaraveendran kwa moyo wako wa pekee”


Source: Millardayo.com

No comments

+255716829257