Mbunge wa Serengeti ahamia CCM
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimepata pigo jingine baada ya kuondokewa na diwani wake na Mbunge wake na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM.
Aliyehama ni Mbunge wa Serengeti mkoa wa Mara kwa tiketi ya CHADEMA, Marwa Ryoba ambaye amejiuzulu nafasi yake ya Ubunge na kuhama CHADEMA kisha kujiunga na CCM kwa madai ya kuamua kuunga jitihada za Rais Dr John Pombe Magufuli.
Wilson Nanyaro
Hata hivyo taarifa za kuondoka kwa Marwa zinaambatana na taarifa za Diwani waCHADEMA kata ya Nkoanekoli halmashauri ya wilaya ya Meru, Wilson Nanyaro nae kutangaza kujiuzulu kama ilivyo kwa Marwa na kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM kwa sababu zile zile za kumuunga mkono Rais DR John Pombe Magufuli.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
No comments
+255716829257