Habari mpya

Roma Mkatoliki ameahidi kutoa wimbo mpya endapo Mexico atamfunga Brazil leo

Katika msimu huu wa kombe la dunia mwaka 2018 msanii kutoka kwenye game ya Bongo Fleva Roma Mkatoliki kupitia ukurasa wake wa twitter ameahidi kutoa ngoma mpya endapo timu ya Brazil itafungwa leo ikiwa inacheza dhidi ya Mexico.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Roma Mkatoliki ambaye yeye ni shabiki wa Brazil katika fainali hizi za Kombe la Dunia, ametoa ahadi hiyo baada ya kuandika “Brazil tukifungwa leo tukitolewa naachia ngoma mpya, Tukishinda tukiwafunga Mexico sitoi ngoma”
Brazil leo jioni anacheza mchezo wake wa mtoano dhidi ya timu ya taifa ya Mexico na mshindi lazima apatikane ambaye atakuwa kakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la dunia kwa mwaka 2018.

No comments

+255716829257