Habari mpya

Baada ya kipigo cha 3-2 kutoka Ubelgiji, hiki ndio walichokifanya Japan

Usiku wa July 2 2018 ulichezwa mchezo wa sita wa hatu ya 16 bora ya World Cup 2018kati ya timu ya taifa ya Ubelgiji dhidi ya timu ya taifa ya Japan katika uwanja wa Rostovnchini Urusi yanapofanyika michuano ya World Cup 2018.
Japan ambao walipita kwa kipengele cha fair play na kuiacha Senegal ikiaga michuano hiyo, licha ya kuanza kupata magoli mawili ya mapema kupitia kwa Haraguchi dakika ya 48 na Inui dakika ya 52, mchezo ulibadilika na Ubelgiji kupindua matokeo kwa kufunga magoli matatu.
Ubelgiji walipata magoli dakika ya 69 kupitia kwa Vertonghen, dakika ya  74 kupitia kwa Fellaini na mwisho dakika nne za nyongeza Chadli akafunga goli la ushindi kwa Ubelgijina Japan kuaga michuano hiyo kwa kipigo cha jumla ya magoli 3-2.
Baada ya game mashabiki wa Japan waliokuwepo katika uwanja wa Rostov walionesha tabia ya kushangaza kwa kuendelea na utamaduni wao wa kusafisha uwanja eneo walilokuwa wameakaa na kuliacha safi kitu ambacho ni nadra kutokea wakati wachezaji wa Japan nao wakaacha dressing room yao wameisafisha na kuacha ujumbe ulioandikwa kwa lugha ya kirusi ila una maana ya “Asante”

Ujumbe ulioachwa na wachezaji wa Japan katika vyumba vya kubadilishia nguo ulioandikwa kirusi ila una maana ya ‘Asante”

1 comment:

+255716829257