Habari mpya

Baunsa wa Diamond apata ajali mbaya

Mlinzi (baunsa) wa Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter amepata ajali mbaya alfajiri ya leo, eneo la Afrikana jijini Dar es Salaam na kupelekwa katika Hospitali ya Lugalo kisha kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Akizungumza kwa taabu hospitalini hapo, Mwarabu Fighter amesema alikuwa amepanda bodaboda ambayo dereva wake akiwa analipita caterpillar, ghafla mbele yao alitokea dereva mwingine wa bodaboda na kusababisha ajali hiyo. Anaeleza kwamba alipoteza fahamu kwa zaidi ya dakika ishirini kutokana na kutokwa na damu nyingi lakini anawashukuru madaktari kwa jinsi walivyompigania.
TAZAMA VIDEO HAPO CHINI AKIHOJIWANA WAANDISHI WA HABARI HOSPITALINI MHIMBILI

No comments

+255716829257