SHERIA YA WAENDESHA BAISKELI KATIKA MAKUTANO YA BARABARA.

Na
Ramadhani Gidion.
Punguza mwendo na kuwa
makini zaidi kwenye makutano kwa sababu madereva wanaweza wasikuone. Kamwe
usiamini kuwa madereva wanakuona. Iwapo utaona kuwa makutano hayo yana magari mengi
na vigumu kupita, simama na ushuke kisha
tembea na baiskeli yako kuvuka barabara, fuata sehemu ambayo watembea kwa miguu
wengine wanapita. Angalia magari yanayopinda mbele yako.
Angalia madereva wanaotoka
pembeni mwa barabara wanaweza wasikuone. Usiendeshe upande wa magari
yanayoashiria au kupunguza mwendo kupinda kushoto madereva wa magari makubwa na marefu wakati
mwingine hushindwa kuona kuwa wamekupita vizuri kabla ya kupinda kushoto.
Kupinda
kulia, Unapopinda kulia, angalia magari yaliyo nyuma yako, onyesha ishara
inayofaa, na iwapo ni salama nenda katikati ya barabara. Subiri hadi kunapokuwa
na upenyo ambao ni salama barabarani kabla ya kumalizia kupinda.
Mzunguko,
Chukua tahadhari kubwa kwenye mzunguko kwani mara nyingi madereva hushindwa kuwaona
na kuwaruhusu waendesha baiskeli. Kwa ujumla ni salama kukaribia mzunguko kwa
njia iliyo upande wa kushoto na kuendelea kupita kushoto kwenye mzunguko hicho chukua
tahadhari kubwa wakati unaendesha kupitia sehemu ya kutokea, na unaweza
kuhitaji kuashiria kulia kuwaonyesha madereva kuwa hutoki kwenye mzunguko.
Angalia magari
yanayokatisha kwenye njia yako kuondoka au kuingia kwenye mzunguko. Mara zote
ni salama kuyaacha magari marefu kupita kwenye mzunguko kabla ya kuendelea.
Iwapo huna uhakika unaweza kuendesha kwa usalama kwenye mzunguko, simama na
shuka kwenye baiskeli na utembee nayo kwenye njia ya watembea kwa miguu.
Tumia Kanuni za Uvukaji
wakati unapita kwenye barabara ya kuingilia. Ishara zinazoongoza makutano.
Fuata maelekezo yanayotolewa na ishara ya taa za barabarani. LAZIMA usimame
iwapo ishara ya Highway Code-Inside-Swa.indd Sec1:12 ighway
Code-Inside-Swa.indd Sec1:12 9/25/08 3:14:42 PM /25/08 3:14:42 PM 13 taa
nyekundu au za njano itaonyeshwa.
Simama kwenye sehemu iliyoandikwa SIMAMA au fuata
nafasi yako kwenye mstari wa magari yanayosubiri.
Chanzo:Kanuni
za barabara,wizara ya miundombinu 2008,Tanzania.
No comments
+255716829257