JIFUNZE KUPIKA KABICHI ZA MAYAI..

Kabichi ni
aina ya mboga za majani ambayo hupikwa kwa
mapishi tofauti. Unaweza kupika kabichi yenyewe bila kuchanganya na
chochote pia unaweza kupika kwa
kuchanganya na nyama, mayai au chochote unachoona kinafaa mboga yako itakuwa nzuri na kuweza kuliwa na ugali, wali na hata
kupikia pilau.
Leo tutaangalia jinsi ya kupika kabichi
iliyochanganywa na mayai, ambapo tunaanza na mahitaji pamoja na hatua za kufuata katika upikaji wa kabichi
iliyochanganywa na mayai.
-MAHITAJI
·
Kabichi moja ya ukubwa wa wastani
·
Mayai manne (4)
·
Mafuta robo lita
·
Vitunguu vinne (4)
·
Karoti kubwa moja
·
Pilipili manga kiasi
·
Chumvi kiasi kwa ladha
JINSI YA
KUPIKA KABICHI HATUA KWA HATUA
1. Chukua kabichi ulikatekate kisha
ulioshe.
2. Washa jiko lolote ulilonalo liwe la
mkaa, gesi au umeme.
3. Kisha bandika kabichi
ulilolikatakata na kuliosha liache liive kidogo kisha ipua.
4. Menya nyanya, katakata vitunguu,
karoti uviweke tayari kwa mapishi.
5. Bandika sufuria jikoni na utie
mafuta ya kupikia, yakipata moto tia vitunguu ukaange mpaka vibadilike rangi
kisha tia nyanya ukaange.
6. Nyanya zikishaiva tia karoti kaanga
kidogo.
7. Baada ya hapo tia pilpili manga
pamoja na kabichi ulilolichemsha.
8. Vunja mayai uliyoandaa na kisha
changanya na kabichi ililoungwa tayari na ukoroge hadi mboga yako ikauke.
Mpaka
kufikia hapo mboga yetu ya kabichi iliyochanganywa na mayai itakuwa imeiva na tayari
kwa kuliwa kwa chakula ukipendacho iwe ugali, wali hata pilau.
No comments
+255716829257