Habari mpya

WATU 11 WAFARIKI KWENYE AJALI YA NDEGE NGORONGORO..

Habari hii imeshtua wengi ambapo katika  kumbukumbu itakua ni Ndege ndogo ya 3 kuanguka Tanzania ndani ya mwaka 2017 lakini hii ndio imechukua uhai wa watu wengi zaidi.
Jeshi la Polisi Arusha limesema ajali ya Ndege ndogo ya Coastal Aviation imetokea kati ya saa 5 na saa 6 asubuhi eneo la Embakazi Wilayani Ngorongoro ikiwa na watu 11 akiwemo Rubani na wote kufariki.
Kabla ya kuanguka ndege hiyo ilipaa kutoka uwanja mdogo wa Arusha saa nne na dakika 10 asubuhi kuelekea uwanja wa Ndege Kilimanjaro (KIA) na kuchukua abiria watano jumla ikawa na abiria 10 na Rubani wa 11.

Majina ya waliokuwemo kwenye Ndege
“Ndege ina chombo maalum cha kurekodi matukio uchunguzi ukifanyika tutajua chanzo kilikua ni nini, miili imeshabainika na kesho tunafanya utaratibu wa kuisafirisha kuja Arusha mjini”
“Ili kuepuka vyombo vinavyohusika viwe vinafanya ukaguzi ili kuepusha ajali sababu muda sio mrefu ilitokea ajali ya ndege ndogo hapa Arusha na iliwahi kutokea nyingine kule mkoani Mara, ni matukio yaliyotokea karibukaribu, vyombo husika vifanye ukaguzi ili kuepusha haya”
Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema chanzo cha ajali hiyo ni hali mbaya ya hewa iliyosababisha Ndege hiyo kupata ajali kwenye Mlima… tunaendelea kufatilia kupata taarifa za chanzo, R.I.P kwa wote waliofariki.

No comments

+255716829257