Habari mpya

ARSENAL YATOA SARE NA PSG NYUMBANI EMIRATES..

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya Makundi imeendelea tena usiku wa November 23 kwa michezo nane kupigwa, michuano hiyo inaendelea baada ya jana November 22 kuchezwa michezo mingine nane ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya Makundi.
3ab30a7300000578-3965922-image-a-10_1479935751360
Mchezo kati ya Arsenal dhidi ya Paris Saint Germain ya Ufaransa ulikuwa ni moja kati ya michezo nane iliyochezwa usiku wa November 23, PSG wakiwa Emirates waliutawala mchezo kwa asilimia 52 dhidi ya wenyeji wao Arsenal waliokuwa wameutawala mchezo kwa asilimia 48.
3ab30cee00000578-3965922-image-a-8_1479935705104
Arsenal wakiwa nyumbani wamelazimishwa sare goli 2-2, magoli ya Arsenal yakifungwa na Oliver Giroud dakika ya 45 na dakika ya 59 Marco Verratti alijifunga, wakati magoli ya PSG yalifungwa na Edinson Cavani dakika ya 18 na goli lao la pili lilipatikana baada ya beki wa Arsenal Alex Iwobi kujifunga kwa kichwa dakika ya 77.

No comments

+255716829257