Habari mpya

WAZAZI WAASWA KUACHA KUWAPA MAZIWA YA KOPO NA YA NG`OMBE WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MWAKA MMOJA..

 
Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuacha kutumia maziwa ya kopo na ya Ng’ombe kwa watoto ambao hawajafikisha mwaka mmoja ili kuwanusuru katika tatizo la kuchubuka utumbo.
Ushauri huo ulitolewa jijini Dar es salaam na kaimu mkurugenzi kitengo cha afya ya uzazi na mtoto, Dk. Georgina Msemo, katika maadhimisho ya unyonyeshaji yanaayoendelea.
Dk Msemo alisema maziwa ya ng’ombe yana Casein ambayo haifai kwa mtoto mwenye umri wa kuzaliwa hadi mwaka mmoja pia alisema maziwa hayo husababisha mzio, pumu na kusema kwamba maziwa ya mama ni bora na yanayotoa kinga ya mwili kwa mtoto katika maisha yake yote.
Dk Msemo amesema ………..>>>Maziwa ya mama ni chakula bora kwa mtoto, kwani licha ya kumpa lishe bora pia humpatia mtoto majianayoyahitaji kwa ukuaji wake katika miezi sita ya mwanzo
>>>’Maziwa mazito na ya njano ambayo huitwa kolostramu yanayotoka siku chache za mwanzo humkinga mtoto dhidi ya maradhi mengi:-Dk Msemo.

No comments

+255716829257