ULIMWENGU WA SOKA: YANAYOJIRI KATIKA USAJILI..
Timu ya Rubin Kazan imemsajili
kiungo Alex Song bure kwa mkataba wa mitatu kutoka kwa miamba wa
Hispania Barcelona. Song aliitumika West Ham msimu uliopita kwa mkopo
baada ya kukosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha Barcelona.
Klabu ya Southampton imemsajili golikipa Alex McCarthy kwa mkataba wa
miaka mitatu toka timu ya Crystal Palace. McCarthy, alicheza michezo
saba msimu uliopita akiwa na klabu yake ya Crystal Palace huu ni usajili
wa tatu wa Watakatifu hao wa Southampton baada ya kuwasajili Nathan
Redmond Pierre-Emile Hojbjerg.Nae beki Steven Taylor amejiunga na timu ya Portland Timbers, inayoshiriki ligi ya kuu ya Marekani akitokea Newcastle United. Beki amekaa kwenye klabu ya Newcastle kwa muda wa 21 toka akiwa mdogo, na amecheza michezo 268.
No comments
+255716829257