HIVI NDIVYO MUSEVENI ALIVYOTANIWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII BAADA YA KUPOKEA SIMU BARABARANI..
Baada ya kuchapishwa kwa picha ya rais wa Uganda Yoweri Museveni, akipokea simu kando ya barabara.
Maelfu ya waganda wamechukulia tukio hilo kwa ucheshi mno hata wengine utundu..
Wengine wanasambaza picha hiyo wakihoji kwanini rais mwenye heshma na taadhima kama yake, anatumia mali ya umma kwa namna hiyo
''eti kwanini maafisa hao wote wa usalama wanalazimishwa kusimama eti bwana Museveni azungumze na mpenzi wake Bi Janeth ilhali wangekutana naye jioni nyumbani ?
Wengine wanahoji kama hilo halikuwa tukio la kujipigia debe eti kwasababu serikali imetengeneza barabara hiyo inayounganisha Uganda na nchi jirani ya Tanzania?
Je hakukuwa na maswala mengine muhimu ya kitaifa ya kujadiliwa ?
Wengine hata walimshangaa kiongozi huyo ambaye alikuwa akitumia simu ya bei nafuu isiyo ya kisasa!
Mmoja wa maafisa wake wa uhusiano mwema bwana Don Wanyama ndiye aliyetibua mjadala huo alipochapisha kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook
kuwa rais Museveni alikuwa amesimamisha msafara wake kwa dakika thelathini ilikupokea simu muhimu faraghani.
Wanyama hakueleza kwanini Museveni aliketi kandakando mwa barabara hiyo muhimu lakini
Waganda walibuni sababu zao kwenye mitandao ya kijamii wengi wakimgoa na kumtania kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 71.
No comments
+255716829257