Habari mpya

HII NDIYO PASS PORT MPYA YA MATAIFA YA AFRIKA..

Hivi karibuni viongozi wa bara la Afrika walizindua hati maalum ya kusafiria ya Afrika mjini Kigali, Rwanda katika kongamano la viongozi wa Afrika. 
Baada ya hati kuzinduliwa watu wa kwanza kupewa walikuwa viongozi wenye hadhi ya kidiplomasia na umoja wa Afrika unatarajia kuwa mataifa ya Afrika yataanza kutoa hati hizo mpya za kusafiri kwa raia kufikia mwaka wa 2018.
Leo July 20 2016 Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi, Augustine Mahiga, amezungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika mkutano wa 27 wa Umoja wa nchi za Afrika uliofanyika hivi karibuni Kigali nchini Rwanda.
Balozi Mahiga amasema kuwa katika mkutano huo ambao walizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo hati ya kusafiria Afrika (passport), ambayo itawezesha watu wa bara hilo kusafiri katika nchi zote za Afrika.
Balozi Mahiga aliongeza kuwa, lengo la kuanza kutumia hati hiyo ya kusafiria kwa nchi za Afrika ni kutoa vikwazo vilivyokuwepo wakati wa kutembelea na kusafiri ndani ya nchi hizo.
Aidha, Balozi Mahiga amesema kwamba, kutolewa kwa hati ya kusafiria ya Afrika ni ishara ya Umoja na mshikamano, hati hizo zimeanza kutolewa kwa marais na viongozi wa Serikali wa nchi ambazo zilihudhuria mkutano huo. Hati hizo zitatumika kwa kuzingatia sheria za kila nchi.

No comments

+255716829257