TANZANIA YATUNUKIWA TUZO NA UMOJA WA NCHI ZA AFRIKA..
July 20
2016 Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi,
Augustine Mahiga, amezungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo
yaliyojadiliwa katika mkutano wa 27 wa Umoja wa nchi za Afrika
uliofanyika hivi karibuni Kigali nchini Rwanda.
Waziri
mahiga amesema Serikali ya Tanzania imepewa tuzo 2 za masuala ya Ustawi
wa Jamii pamoja na ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi ya maamuzi ya
Serikali na Taasisi mbalimbali katika Mkutano wa 27 wa Umoja wa Nchi
za Afrika (AU) uliofanyika hivi karibuni Kigali nchini Rwanda……..
>>>’Tanzania
imetambuliwa na AU kama nchi ambayo kwa miaka 15 sasa imekua na
mikakati mbalimbali ya kitaifa ya kuzingatia haki za wanawake na
kutimiza malengo ya milenia’
Waziri Mahiga aliongeza kuwa Tanzania ni kati ya nchi tano bora katika bara la Afrika ambazo zimepewa tuzo hizo.
No comments
+255716829257