EURO 2016: UFARASA YATINGA FAINALI..

Ufaransa imetinga katika hatua fainali ya Kombe la Mataifa barani Ulaya kwa mwaka huu baada ya kuifunga Ujerumani 2 - 0.
Mshambuliaji
Antoine Griezmann ndiye aliyeipeleka timu yake ya Ufaransa katika hatua
fainali ya Kombe la Mataifa barani Ulaya kwa mwaka huu baada ya
kuifungia magoli 2 na kuishangaza Ujerumani iliyokuwa imetawala mchezo
huo wa nusu fainali.Mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid alianza kwa kuandika bao la kwanza kwa njia ya penalti katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza kabla ya kupachika bao la pili na ushindi kipindi cha pili baada ya golikipa wa Ujerumani Manuel Neuer kufanya makosa golini.
Kwa matokeo hayo sasa Ufaransa mwenyeji wa michuano hiyo itakutana na Ureno katika mechi ya fainali siku ya Jumapili.
No comments
+255716829257